#Glm news| Joh Makini ataja sababu ya kuchelewa kuachiwa kwa wimbo wa Weusi na Sauti Sol

Rapper wa kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka sababu ya kuchelewa kwa wimbo wao na Sauti Sol kutoka Kenya.

Mwezi Septemba mwaka jana, Joh alithibitisha kupitia mtandao wa Instagram kuwa wimbo huo ungetoka kabla mwaka huo haujaisha lakini mpaka sasa bado haujatoka.

Akiongea na Bongo5, Joh amesema sababu ya kuchelewa kutoka kwa wimbo huo ni kutokana na baadhi ya marekebisho yaliyokuwa yanatakiwa kufanyika katika wimbo huo ambapo wote kwa pamoja walikuwa busy na kazi nyingine.

“Sauti Sol kama ambavyo unawafuatilia utagundua ni watu ambao wako busy sana na sisi pia hivyo hivyo. Ngoma tulishaifanya lakini kama wasanii pia tuligundua kuna vitu turekebishe. Hiyo ndio sababu kubwa na sasa ipo tayari,” amesema Joh.

“Mipango ya video ikiwa tayari na vile ambavyo sote tutakua tayari itoke. I mean sisi na Sauti Sol ili tuweze kupromote kwa pamoja isiwe kwa upande mmoja,” ameongeza.