#Glm News| Christine Wawira – Afuata nyayo za Lupita Nyon’o Marekani

Christine Wawira ni miongoni mwa waigizaji wanaochipukia kwa kasi katika uwanda wa Hollywood nchini Marekani na kuweza kuungana na Mkenya mwenzake Lupita Nyong’o ambaye tayari amejipatia umaarufu zaidi kupitia filamu ya “12 Years In A Slave”

Image result for "12 Years In A Slave" cover

Lupita amefika mbali hadi kunyakua tuzo ya Oscar.

Akihojiwa na gazeti la Burudani kwa njia ya Twitter kutoka Los Angeles Marekani anakoishi kwa sasa Christine anasema kabla ya kuibukia huko, alizaliwa Desemba 20, 1987 Nairobi Kenya.

Muigizaji huyo ambaye jina lake la zamani Naila Pierce kabla hajabadili na kuitwa Christine, anasema mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka saba walihamia London, Uingereza pamoja na wazazi wao na mdogo wake wa kike kabla hawajapasua anga mpaka Atlanta, Marekani.

Christine ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne wa mchungaji wa Wawira Njagi lakini naye ni mama wa watoto wawili. ” Nilianza kuigiza nikiwa na umri wa miaka 14 na nilifurahia sana kwakuwa nilikuwa najua nini natarajia kufanya katika maisha yangu” anaeleza Christine.

Tayari ameanza kuonyesha makali katika fani hiyo kupitia filamu alizocheza ambazo zimeingia sokoni na kufanya vizuri filamu hizo ni Tough Call, Sign of The Dragon, Deadbeat na alishiriki katika sehemu ya tamthilia ya Modern Family.