#Glm News| Diamond – usiogope maneno Harmonize

Msanii Diamond Platinumz na mmiliki wa label ya WCB, Diamond Platnumz amempa ushauri msaanii wa kwanza kusainiwa katika label hiyo, Harmonize kuhusu maneno ya watu.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Eneka’, kupitia mtandao wa Instagram amemtaka Harmonize kutoogopa maneno ya watu katika kazi zake.

Me telling @harmonize_tz “Usiogope Maneno maana Maneno Asili yake Uswazi, na Uswahilini ndipo Tulipozaliwa na kulelewa… Chamuhimu Tuendelee kupambana na tuzidi kuuwashika mkono wenzetu kutoka kwenye mtaa, ili Mabishoo, na Watoto wakishua wazidi kuchukia….! @wcb_wasafiFor life!

Me telling @harmonize_tz “Fu***k all the haters!” , we are famous, Powerful & Rich!…..@wcb_wasafi for life!!! please tag my all @wcb_wasafi family…..

Ikumbuke siku ya Ijumaa (July 28) kupitia mtandao huo Diamond Platnumz aliwajia juu watu ambao wadai uhusianao wake na Baby Mama wake, Zari TheBoss Lady umevunjika na kutumia maneno makali kuwaeleza kuwa bado wapo pamoja.