#Glm_movies|KAJALA ALIA MWISHO WA MWAKA!

MKALI wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa, anaona mwaka ndiyo unaisha, lakini bado hajatimiza malengo yake aliyojipangia, jambo ambalo linamuumiza kichwa.

Kajala aliiambia Over Ze Weekend kuwa, mwaka huu haukuwa mzuri kwani vitu vingi vilikuwa haviendi sawa hivyo alijikuta anashindwa kutimiza malengo aliyojiwekea.

“Kiukweli sijatimiza malengo yangu hata kidogo, naumia mno kwa vile pia mwaka ulikuwa mgumu mno na pesa zilikuwa hazionekani,” alisema Kajala.

 

Glp